Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Isaya 65:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri, watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’ Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri, watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’ Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri, watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’ Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana katika kishada cha zabibu, nao watu husema, ‘Usikiharibu, kwa kuwa bado kuna baraka ndani yake,’ hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hili ndilo asemalo bwana: “Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana katika kishada cha zabibu, nao watu husema, ‘Usikiharibu, kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’ hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Isaya 65:8
14 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.

Kama BWANA wa majeshi asingalituachia mabaki machache sana, tungalikuwa kama Sodoma, tungalifanana na Gomora.

Mabaki, nao ni mabaki ya Yakobo, watamrudia Mungu, aliye mwenye nguvu.

Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki.

kwa ajili ya jina langu nitaahirisha hasira yangu, na kwa ajili yako nitajizuia, ili nisifiwe, wala nisikukatilie mbali.

Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.

Maana mimi ni pamoja nawe, asema BWANA, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.

Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?

Na kama siku hizo zisingalifupishwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupishwa.

Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.