na juu ya mifugo iliyolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya mifugo iliyokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai;
Isaya 65:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho, bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugo kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. Biblia Habari Njema - BHND Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho, bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugo kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho, bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugo kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. Neno: Bibilia Takatifu Sharoni itakuwa malisho kwa ajili ya makundi ya kondoo, na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia kwa makundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta. Neno: Maandiko Matakatifu Sharoni itakuwa malisho kwa ajili ya makundi ya kondoo, na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia kwa makundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta. BIBLIA KISWAHILI Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. |
na juu ya mifugo iliyolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya mifugo iliyokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai;
Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hadi mipakani mwake.
Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani.
Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA, ukuu wa Mungu wetu.
Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta BWANA; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa.
BWANA wa majeshi asema hivi, Katika mahali hapa, palipo ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, na katika miji yake yote, yatakuwapo makao ya wachungaji wakiwalaza kondoo wao.
Nami nitamleta Israeli tena malishoni kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya milima ya Efraimu, na katika Gileadi.
Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.