Isaya 64:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Laiti ungepasua mbingu, na kushuka, ili milima itetemeke mbele zako; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Laiti ungalizipasua mbingu ukashuka chini, milima ikakuona na kutetemeka kwa hofu! Biblia Habari Njema - BHND Laiti ungalizipasua mbingu ukashuka chini, milima ikakuona na kutetemeka kwa hofu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Laiti ungalizipasua mbingu ukashuka chini, milima ikakuona na kutetemeka kwa hofu! Neno: Bibilia Takatifu Laiti ungepasua mbingu na kushuka chini, ili milima itetemeke mbele zako! Neno: Maandiko Matakatifu Laiti ungelipasua mbingu na kushuka chini, ili milima ingelitetemeka mbele zako! BIBLIA KISWAHILI Laiti ungepasua mbingu, na kushuka, ili milima itetemeke mbele zako; |
Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.
Kwa nini mataifa yaseme, Yuko wapi Mungu wao? Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika Kijulike kati ya mataifa machoni petu.
wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote.
nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi.
Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo huyo alimaye atamfikia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.
Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Nili, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri.
Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.
Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake;
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.