Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Isaya 63:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa nini mavazi yako ni mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mbona nguo yako ni nyekundu, nyekundu kama ya mtu anayekamua zabibu? Biblia Habari Njema - BHND Lakini mbona nguo yako ni nyekundu, nyekundu kama ya mtu anayekamua zabibu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mbona nguo yako ni nyekundu, nyekundu kama ya mtu anayekamua zabibu? Neno: Bibilia Takatifu Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu? Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu? BIBLIA KISWAHILI Kwa nini mavazi yako ni mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu? |
Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Akajivika haki kama deraya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho.
Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.
Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitakuweka tayari kwa damu, na damu itakufuatia; ikiwa hukuchukia damu, basi damu itakufuatia.
Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.
Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kwa upanga huo awapige mataifa. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.