Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alilovikwa na mamaye, Siku ya posa yake, Siku ya furaha ya moyo wake.
Isaya 62:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana, ndivyo aliyekujenga atakavyokuwa mume wako. Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi, ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako. Biblia Habari Njema - BHND Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana, ndivyo aliyekujenga atakavyokuwa mume wako. Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi, ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana, ndivyo aliyekujenga atakavyokuwa mume wako. Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi, ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo Mwashi wako atakavyokuoa; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo wanao watakavyokuoa wewe; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. BIBLIA KISWAHILI Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana harusi amfurahiavyo bibi harusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. |
Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alilovikwa na mamaye, Siku ya posa yake, Siku ya furaha ya moyo wake.
Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni, Pamoja nami toka Lebanoni. Shuka kutoka kilele cha Amana, Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni; Kutoka mapangoni mwa simba, Kutoka milimani mwa chui.
Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.
Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikika ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.
Naam, nitafurahi juu yao niwatendee mema, nami nitawapanda katika nchi hii kweli kweli, kwa moyo wangu wote, na kwa roho yangu yote.
Nami nitakuposa uwe wangu wa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema BWANA; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi;
BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.
Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.