Isaya 62:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utakuwa taji zuri mkononi mwa Mwenyezi-Mungu; kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Biblia Habari Njema - BHND Utakuwa taji zuri mkononi mwa Mwenyezi-Mungu; kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utakuwa taji zuri mkononi mwa Mwenyezi-Mungu; kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Neno: Bibilia Takatifu Utakuwa taji la fahari mkononi mwa Mwenyezi Mungu, taji la kifalme mkononi mwa Mungu wako. Neno: Maandiko Matakatifu Utakuwa taji ya fahari mkononi mwa bwana, taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako. BIBLIA KISWAHILI Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. |
Katika siku ile BWANA wa majeshi atakuwa ni taji la fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake.
Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.
Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji la kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?