Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Isaya 61:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Watayajenga upya magofu ya zamani, wataisimika miji iliyoharibiwa hapo kwanza; wataitengeneza miji iliyobomolewa, uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Watayajenga upya magofu ya zamani, wataisimika miji iliyoharibiwa hapo kwanza; wataitengeneza miji iliyobomolewa, uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Watayajenga upya magofu ya zamani, wataisimika miji iliyoharibiwa hapo kwanza; wataitengeneza miji iliyobomolewa, uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Watajenga upya magofu ya zamani na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani; watafanya upya miji iliyoharibiwa, iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Watajenga upya magofu ya zamani na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani; watafanya upya miji iliyoharibiwa, iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Isaya 61:4
11 Marejeleo ya Msalaba  

Maana sisi tu watumwa; lakini Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikishia rehema zake, mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutupa maisha mapya, kuisimamisha nyumba ya Mungu wetu, na kuitengeneza palipobomoka, na atulinde katika Yuda na Yerusalemu.

Njoni muyatazame matendo ya BWANA, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.

Upite na kupaona palipoharibika milele; Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.

Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu.

Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejesha njia za kukaa.

Ni siku ya kujengwa kuta zako! Siku hiyo mpaka utasongezwa mbali.

Piga kelele tena, na kusema, BWANA wa majeshi asema hivi, Miji yangu itajawa na ufanisi tena; naye BWANA ataufariji Sayuni tena, atauchagua Yerusalemu tena.