Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.
Isaya 60:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni nani hawa warukao kama wingu, Na kama njiwa waendao madirishani kwao? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nani hao wanaopepea kama mawingu, kama njiwa wanaoruka kwenda viotani mwao? Biblia Habari Njema - BHND Nani hao wanaopepea kama mawingu, kama njiwa wanaoruka kwenda viotani mwao? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nani hao wanaopepea kama mawingu, kama njiwa wanaoruka kwenda viotani mwao? Neno: Bibilia Takatifu “Ni nani hawa warukao kama mawingu, kama hua kuelekea kwenye viota vyao? Neno: Maandiko Matakatifu “Ni nani hawa warukao kama mawingu, kama hua kuelekea kwenye viota vyao? BIBLIA KISWAHILI Ni nani hawa warukao kama wingu, Na kama njiwa waendao madirishani kwao? |
Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.
Ndipo utasema moyoni mwako, Ni nani aliyenizalia watoto hawa, na mimi nimefiwa na watoto wangu, nami niko peke yangu, nimehamishwa, ninatangatanga huko na huku? Tena ni nani aliyewalea hawa? Tazama, niliachwa peke yangu; hawa je! Walikuwa wapi?
Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani.
Watakuja wakitetemeka kama shomoro, toka Misri, na kama hua, toka nchi ya Ashuru; nami nitawakalisha katika nyumba zao, asema BWANA.
Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.
Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;