Isaya 60:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa utukufu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Hutahitaji tena jua kukuangazia mchana, wala mwezi kukumulikia usiku; maana mimi Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa fahari yako. Biblia Habari Njema - BHND “Hutahitaji tena jua kukuangazia mchana, wala mwezi kukumulikia usiku; maana mimi Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa fahari yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Hutahitaji tena jua kukuangazia mchana, wala mwezi kukumulikia usiku; maana mimi Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa fahari yako. Neno: Bibilia Takatifu Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako. Neno: Maandiko Matakatifu Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana bwana atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako. BIBLIA KISWAHILI Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa utukufu wako. |
Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?
Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Katika siku ile BWANA wa majeshi atakuwa ni taji la fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake.
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.
Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia BWANA, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli.
Nao waliokombolewa na BWANA watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.
Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza.
Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.
Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma.
Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.
Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.
Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.