Isaya 60:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Badala ya shaba nitaleta dhahabu, Na badala; ya chuma nitaleta fedha, Na badala ya mti, shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena nitaifanya amani kuwa kama msimamizi wako, Na haki kuwa kiongozi wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Badala ya shaba nitakuletea dhahabu, badala ya chuma nitakuletea fedha, badala ya miti, nitakuletea shaba, na badala ya mawe nitakuletea chuma. Amani itatawala juu yako, uadilifu utakuongoza. Biblia Habari Njema - BHND “Badala ya shaba nitakuletea dhahabu, badala ya chuma nitakuletea fedha, badala ya miti, nitakuletea shaba, na badala ya mawe nitakuletea chuma. Amani itatawala juu yako, uadilifu utakuongoza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Badala ya shaba nitakuletea dhahabu, badala ya chuma nitakuletea fedha, badala ya miti, nitakuletea shaba, na badala ya mawe nitakuletea chuma. Amani itatawala juu yako, uadilifu utakuongoza. Neno: Bibilia Takatifu Badala ya shaba nitakuletea dhahabu, na fedha badala ya chuma. Badala ya mti nitakuletea shaba, na chuma badala ya mawe. Nitafanya amani kuwa mtawala wako, na haki kuwa mfalme wako. Neno: Maandiko Matakatifu Badala ya shaba nitakuletea dhahabu, na fedha badala ya chuma. Badala ya mti nitakuletea shaba, na chuma badala ya mawe. Nitafanya amani kuwa mtawala wako, na haki kuwa mfalme wako. BIBLIA KISWAHILI Badala ya shaba nitaleta dhahabu, Na badala; ya chuma nitaleta fedha, Na badala ya mti, shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena nitaifanya amani kuwa kama msimamizi wako, Na haki kuwa kiongozi wako. |
nami nitawarejesha tena waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza, na washauri wako kama hapo mwanzo; baada ya hayo utaitwa, Mji wa haki, mji mwaminifu.
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.
Badala ya michongoma utamea msonobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.
Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.
Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako, Ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako; Bali utaziita kuta zako, Wokovu, Na malango yako, Sifa.
Ndipo badala yake atasimama mmoja, atakayepitisha mwenye kutoza ushuru kati ya utukufu wa ufalme wake; lakini katika muda wa siku chache ataangamizwa, si kwa hasira, wala si katika vita.
Katika siku hiyo BWANA atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa BWANA mbele yao.
kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.
Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.