Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
Isaya 60:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu yangu nilikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu asema: “Wageni watazijenga upya kuta zako, wafalme wao watakutumikia. Maana kwa hasira yangu nilikupiga, lakini kwa fadhili yangu nimekuhurumia. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu asema: “Wageni watazijenga upya kuta zako, wafalme wao watakutumikia. Maana kwa hasira yangu nilikupiga, lakini kwa fadhili yangu nimekuhurumia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu asema: “Wageni watazijenga upya kuta zako, wafalme wao watakutumikia. Maana kwa hasira yangu nilikupiga, lakini kwa fadhili yangu nimekuhurumia. Neno: Bibilia Takatifu “Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonesha huruma. Neno: Maandiko Matakatifu “Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonyesha huruma. BIBLIA KISWAHILI Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumia; Maana katika ghadhabu yangu nilikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu. |
Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.
Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;
Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu.
Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Nao walio mbali watakuja na kusaidia kujenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu.
Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.