Isaya 58:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu. Biblia Habari Njema - BHND “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mkifanya hivyo mtang'ara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko na uponyaji wako utatokea upesi; ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, na utukufu wa Mwenyezi Mungu utakuwa mlinzi nyuma yako. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko na uponyaji wako utatokea upesi; ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, na utukufu wa bwana utakuwa mlinzi nyuma yako. BIBLIA KISWAHILI Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde. |
Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao;
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.
Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu BWANA atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.
Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia.
Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika makabila ya watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.
Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.
Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.
Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.
Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.
Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Akamkodolea macho, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.