Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Isaya 57:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mnafikiri mnafanya sawa, lakini nitayafichua matendo yenu, nayo miungu yenu haitawafaa kitu. Biblia Habari Njema - BHND Mnafikiri mnafanya sawa, lakini nitayafichua matendo yenu, nayo miungu yenu haitawafaa kitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mnafikiri mnafanya sawa, lakini nitayafichua matendo yenu, nayo miungu yenu haitawafaa kitu. Neno: Bibilia Takatifu Nitaifunua haki yako na matendo yako, nayo hayatakufaidi. Neno: Maandiko Matakatifu Nitaifunua haki yako na matendo yako, nayo hayatakufaidi. BIBLIA KISWAHILI Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa. |
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.
Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.
Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu.
Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu.
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.
Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;