Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii;
Isaya 56:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wala mgeni, aambatanaye na BWANA, asiseme hivi, Hakika yake BWANA atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mgeni anayenitambua mimi Mwenyezi-Mungu asifikiri: ‘Hakika Mwenyezi-Mungu atanitenga na watu wake.’ Naye towashi asiseme: ‘Mimi ni mti mkavu tu!’ Biblia Habari Njema - BHND “Mgeni anayenitambua mimi Mwenyezi-Mungu asifikiri: ‘Hakika Mwenyezi-Mungu atanitenga na watu wake.’ Naye towashi asiseme: ‘Mimi ni mti mkavu tu!’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mgeni anayenitambua mimi Mwenyezi-Mungu asifikiri: ‘Hakika Mwenyezi-Mungu atanitenga na watu wake.’ Naye towashi asiseme: ‘Mimi ni mti mkavu tu!’ Neno: Bibilia Takatifu Usimwache mgeni aambatanaye na Mwenyezi Mungu aseme, “Hakika Mwenyezi Mungu atanitenga na watu wake.” Usimwache towashi yeyote alalamike akisema, “Mimi ni mti mkavu tu.” Neno: Maandiko Matakatifu Usimwache mgeni aambatanaye na bwana aseme, “Hakika bwana atanitenga na watu wake.” Usimwache towashi yeyote alalamike akisema, “Mimi ni mti mkavu tu.” BIBLIA KISWAHILI Wala mgeni, aambatanaye na BWANA, asiseme hivi, Hakika yake BWANA atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. |
Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii;
Wayahudi wakaagiza na kutadaraki juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, na juu ya wote watakaojiunga nao, isikome, ya kwamba watazishika siku hizo mbili kulingana na andiko lile, na kwa majira yake kila mwaka;
Maana BWANA atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye atawaweka katika nchi yao wenyewe; na mgeni atajiunga nao, nao wataambatana na nyumba ya Yakobo.
Na baadhi ya wana wako utakaowazaa, watakaotoka kwako, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.
Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali.
Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;
Watauliza njia ya kwenda Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njooni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.
au aliye na kibyongo, au aliyedumaa, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;
Tena wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu.
BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.
Nao watataambatana nawe, na kuhudumu katika hema ya kukutania, kwa ajili ya huduma yote ya hema; na mgeni asiwakaribie ninyi.
Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.
Wengine miongoni mwao wakaamini, wakafuatana na Paulo na Sila; na Wagiriki waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Tito Yusto, mcha Mungu, ambaye nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sinagogi.
ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia;