Isaya 54:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana BWANA amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema: Biblia Habari Njema - BHND “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema: Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako. Neno: Maandiko Matakatifu bwana atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako. BIBLIA KISWAHILI Maana BWANA amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. |
Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana hiyo ni sehemu yako ya maisha; na katika kazi zako unazozifanya chini ya jua.
Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.
Nami nitakuposa uwe wangu wa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, ingawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.