Isaya 54:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Minara yako nitaijenga kwa mawe ya akiki, malango yako kwa almasi, na ukuta wako kwa mawe ya thamani. Biblia Habari Njema - BHND Minara yako nitaijenga kwa mawe ya akiki, malango yako kwa almasi, na ukuta wako kwa mawe ya thamani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Minara yako nitaijenga kwa mawe ya akiki, malango yako kwa almasi, na ukuta wako kwa mawe ya thamani. Neno: Bibilia Takatifu Nitafanya minara yako ya akiki, malango yako kwa vito ving’aavyo, nazo kuta zako zote za vito vya thamani. Neno: Maandiko Matakatifu Nitafanya minara yako ya akiki, malango yako kwa vito ving’aavyo, nazo kuta zako zote za vito vya thamani. BIBLIA KISWAHILI Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo. |
Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.
na malango ya mji yatatajwa kwa majina ya makabila ya Israeli, malango matatu upande wa kaskazini; lango la Reubeni, moja; lango la Yuda, moja; na lango la Lawi, moja.
Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.
ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya makabila kumi na mawili ya Waisraeli.