Isaya 51:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC nami nitalitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitawanywesha watesi wako kikombe hicho waliokuambia ulale chini wapite juu yako; wakaufanya mgongo wako kama ardhi, kama barabara yao ya kupitia.” Biblia Habari Njema - BHND Nitawanywesha watesi wako kikombe hicho waliokuambia ulale chini wapite juu yako; wakaufanya mgongo wako kama ardhi, kama barabara yao ya kupitia.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitawanywesha watesi wako kikombe hicho waliokuambia ulale chini wapite juu yako; wakaufanya mgongo wako kama ardhi, kama barabara yao ya kupitia.” Neno: Bibilia Takatifu Nitakiweka mikononi mwa watesi wako, wale waliokuambia, ‘Anguka kifudifudi ili tuweze kutembea juu yako.’ Ukaufanya mgongo wako kama ardhi, kama njia yao ya kupita.” Neno: Maandiko Matakatifu Nitakiweka mikononi mwa watesi wako, wale waliokuambia, ‘Anguka kifudifudi ili tuweze kutembea juu yako.’ Ukaufanya mgongo wako kama ardhi, kama njia yao ya kupita.” BIBLIA KISWAHILI nami nitalitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake. |
Uliwapandisha watu Juu ya vichwa vyetu. Tulipitia motoni na majini; Ukatutoa na kutuleta kwenye ufanisi.
Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kuyumbayumba, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.
Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi BWANA, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu.
Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbayumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.
Na behewa lililo nje ya hekalu uliache nje wala usilipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.