Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
Isaya 50:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mgongo wangu niliwaachia walionipiga, mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu; walioniaibisha na kunitemea mate, sikujificha mbali nao. Biblia Habari Njema - BHND Mgongo wangu niliwaachia walionipiga, mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu; walioniaibisha na kunitemea mate, sikujificha mbali nao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mgongo wangu niliwaachia walionipiga, mashavu yangu waliozing'oa ndevu zangu; walioniaibisha na kunitemea mate, sikujificha mbali nao. Neno: Bibilia Takatifu Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao, mashavu yangu wale wang’oao ndevu zangu; sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha na kutemewa mate. Neno: Maandiko Matakatifu Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao, mashavu yangu wale wang’oao ndevu zangu; sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha na kutemewa mate. BIBLIA KISWAHILI Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate. |
Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.
Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.
Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakamchukua wakampiga makofi.
Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.