Isaya 50:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bwana Mungu amenifanya msikivu, nami sikuwa mkaidi wala kugeuka mbali naye. Biblia Habari Njema - BHND Bwana Mungu amenifanya msikivu, nami sikuwa mkaidi wala kugeuka mbali naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bwana Mungu amenifanya msikivu, nami sikuwa mkaidi wala kugeuka mbali naye. Neno: Bibilia Takatifu Bwana Mungu Mwenyezi amezibua masikio yangu, nami sikuwa mwasi, wala sikurudi nyuma. Neno: Maandiko Matakatifu bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu, nami sikuwa mwasi, wala sikurudi nyuma. BIBLIA KISWAHILI Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma. |
Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniondokee; lakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.
Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
Naye aliyenituma yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.
tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.