Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda mwitu.
Isaya 5:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ole wao wanaojiona kuwa wenye hekima ambao wanajiona kuwa wenye akili. Biblia Habari Njema - BHND Ole wao wanaojiona kuwa wenye hekima ambao wanajiona kuwa wenye akili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ole wao wanaojiona kuwa wenye hekima ambao wanajiona kuwa wenye akili. Neno: Bibilia Takatifu Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe, na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe, na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. BIBLIA KISWAHILI Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe! |
Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda mwitu.
Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa.
Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli.
Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.
Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini kwa kuwa sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.