Isaya 49:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe Siyoni wasema: “Mwenyezi-Mungu ameniacha; hakika Bwana wangu amenisahau.” Biblia Habari Njema - BHND Wewe Siyoni wasema: “Mwenyezi-Mungu ameniacha; hakika Bwana wangu amenisahau.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe Siyoni wasema: “Mwenyezi-Mungu ameniacha; hakika Bwana wangu amenisahau.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Sayuni alisema, “Mwenyezi Mungu ameniacha, Bwana amenisahau.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Sayuni alisema, “bwana ameniacha, Bwana amenisahau.” BIBLIA KISWAHILI Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. |
Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?
Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.
Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?
Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.
Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
Maana BWANA amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako.
basi, kwa hiyo angalieni, nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu;
BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
Na wewe, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli; Ninyi mwasema, Makosa yetu na dhambi zetu ni juu yetu, nasi tumedhoofika katika dhambi hizo; basi tungewezaje kuwa hai?