Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.
Isaya 48:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njoni karibu nami msikie jambo hili: Tangu mwanzo mimi sikusema kwa siri, tangu mambo hayo yaanze kutendeka, nimekuwapo.” Sasa, Bwana Mungu amenituma, na kunipa nguvu ya roho yake. Biblia Habari Njema - BHND Njoni karibu nami msikie jambo hili: Tangu mwanzo mimi sikusema kwa siri, tangu mambo hayo yaanze kutendeka, nimekuwapo.” Sasa, Bwana Mungu amenituma, na kunipa nguvu ya roho yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Njoni karibu nami msikie jambo hili: Tangu mwanzo mimi sikusema kwa siri, tangu mambo hayo yaanze kutendeka, nimekuwapo.” Sasa, Bwana Mungu amenituma, na kunipa nguvu ya roho yake. Neno: Bibilia Takatifu “Nikaribieni na msikilize hili: “Tangu tangazo la kwanza sikusema kwa siri; wakati litokeapo, nitakuwako hapo.” Sasa Bwana Mungu Mwenyezi amenituma, kwa Roho wake Mtakatifu. Neno: Maandiko Matakatifu “Nikaribieni na msikilize hili: “Tangu tangazo la kwanza sikusema kwa siri; wakati litokeapo, nitakuwako hapo.” Sasa bwana Mwenyezi amenituma, kwa Roho wake. BIBLIA KISWAHILI Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake. |
Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi makabila ya watu; dunia na isikie, na chote kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo.
Nyamazeni mbele zangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu.
Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Sikusema kwa siri, katika mahali pa nchi ya giza; sikuwaambia wazao wa Yakobo; Nitafuteni bure; Mimi, BWANA, nasema ukweli; nanena mambo ya haki.
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.