Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Isaya 47:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatangatanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndivyo watakavyokuwa hao uliowategemea hivyo, hao uliojishughulisha nao tangu ujana wako. Watatangatanga kila mmoja njia yake; hakuna hata mmoja atakayeweza kukuokoa.” Biblia Habari Njema - BHND Ndivyo watakavyokuwa hao uliowategemea hivyo, hao uliojishughulisha nao tangu ujana wako. Watatangatanga kila mmoja njia yake; hakuna hata mmoja atakayeweza kukuokoa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndivyo watakavyokuwa hao uliowategemea hivyo, hao uliojishughulisha nao tangu ujana wako. Watatangatanga kila mmoja njia yake; hakuna hata mmoja atakayeweza kukuokoa.” Neno: Bibilia Takatifu Hayo ndiyo yote wanayoweza kuwatendea ninyi, hawa ambao umetaabika nao na kufanya nao biashara tangu utoto. Kila mmoja atatoroka; hakuna yeyote awezaye kukuokoa. Neno: Maandiko Matakatifu Hayo ndiyo yote wanayoweza kuwatendea ninyi, hawa ambao umetaabika nao na kufanya nao biashara tangu utoto. Kila mmoja atatoroka; hakuna yeyote awezaye kukuokoa. BIBLIA KISWAHILI Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatangatanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa. |
Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa kutoka kwa taabu yake.
Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wanajimu, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe kutoka kwa mambo yatakayokupata.
Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.
Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.