Isaya 46:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kumbukeni haya, mkajioneshe kuwa wanaume; jifahamisheni haya, ninyi mkosao; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kumbukeni jambo hili na kutafakari, liwazeni akilini mwenu enyi wakosefu. Biblia Habari Njema - BHND “Kumbukeni jambo hili na kutafakari, liwazeni akilini mwenu enyi wakosefu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kumbukeni jambo hili na kutafakari, liwazeni akilini mwenu enyi wakosefu. Neno: Bibilia Takatifu “Kumbukeni hili, litieni akilini, liwekeni moyoni, enyi waasi. Neno: Maandiko Matakatifu “Kumbukeni hili, litieni akilini, liwekeni moyoni, enyi waasi. BIBLIA KISWAHILI Kumbukeni haya, mkajionyeshe kuwa wanaume; jifahamisheni haya, ninyi mkosao; |
Ukasema, Mimi nitakuwa malkia milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.
Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;
BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu.
Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.
Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kubakiza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu muwe watu wazima.