Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akatengeneza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.
Isaya 46:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu humimina dhahabu kutoka mifuko yao, hupima fedha kwenye mizani zao, wakamwajiri mfua dhahabu atengeneze sanamu kisha huisujudu na kuiabudu! Biblia Habari Njema - BHND Watu humimina dhahabu kutoka mifuko yao, hupima fedha kwenye mizani zao, wakamwajiri mfua dhahabu atengeneze sanamu kisha huisujudu na kuiabudu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu humimina dhahabu kutoka mifuko yao, hupima fedha kwenye mizani zao, wakamwajiri mfua dhahabu atengeneze sanamu kisha huisujudu na kuiabudu! Neno: Bibilia Takatifu Wengine humwaga dhahabu kutoka mifuko yao, na kupima fedha kwenye mizani; huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu, kisha huisujudia na kuiabudu. Neno: Maandiko Matakatifu Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao, na kupima fedha kwenye mizani; huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu, kisha huisujudia na kuiabudu. BIBLIA KISWAHILI Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu. |
Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akatengeneza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.
wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu wakasema, “Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri”.
Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyotengenezwa kwa vidole vyao wenyewe.
Nanyi mtakitia najisi kifuniko cha sanamu zenu za fedha zilizochongwa, na mabamba ya sanamu zenu za dhahabu zilizoyeyushwa; utazitupilia mbali kama kitu kilicho najisi; utasema, Haya, toka hapa.
Jikusanyeni mje; na kukaribia pamoja, ninyi wa mataifa mliookoka; hawana maarifa wale wachukuao mti wa sanamu yao ya kuchonga; wamwombao mungu asiyeweza kuokoa.
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya fundi stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawati na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi wao.
Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu.
Nebukadneza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.
Na sasa wanazidi kufanya dhambi, nao wamejifanyia sanamu kwa fedha yao, naam, sanamu kwa kadiri ya akili zao; zote pia ni kazi ya mafundi; nao huzitaja hivi, Wanaume watoao dhabihu na wazibusu ndama.
Basi, kwa kuwa sisi tu wazawa wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.