Isaya 44:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC nao watachipua kama nyasi, kama mierebi kandokando mwa vijito. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watachipua kama nyasi penye maji mengi, kama majani kandokando ya vijito. Biblia Habari Njema - BHND Watachipua kama nyasi penye maji mengi, kama majani kandokando ya vijito. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watachipua kama nyasi penye maji mengi, kama majani kandokando ya vijito. Neno: Bibilia Takatifu Nao watachipua kama nyasi katika shamba la majani, kama mierezi kando ya vijito vya maji yanayotiririka. Neno: Maandiko Matakatifu Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani, kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo. BIBLIA KISWAHILI nao watachipua kama nyasi, kama mierezi kandokando mwa vijito. |
Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi, Na uzao wako utakuwa kama nyasi za nchi.
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu.
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.
Akatwaa tena mbegu katika mbegu za nchi hiyo, akaipanda katika udongo uzaao sana, akaiweka kando ya maji mengi; aliipandikiza kama mti ukuao karibu na mto.
Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba.
Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya wanaume ikawa kama elfu tano.