Isaya 44:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi-Mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia! Imbeni kwa furaha enyi milima! Enyi misitu na miti yote iliyomo, imbeni. Maana Mwenyezi-Mungu amewakomboa wazawa wa Yakobo, naye atatukuka katika nchi ya Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi-Mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia! Imbeni kwa furaha enyi milima! Enyi misitu na miti yote iliyomo, imbeni. Maana Mwenyezi-Mungu amewakomboa wazawa wa Yakobo, naye atatukuka katika nchi ya Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi-Mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia! Imbeni kwa furaha enyi milima! Enyi misitu na miti yote iliyomo, imbeni. Maana Mwenyezi-Mungu amewakomboa wazawa wa Yakobo, naye atatukuka katika nchi ya Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, kwa maana Mwenyezi Mungu amefanya jambo hili. Ee vilindi vya dunia, piga kelele. Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, enyi misitu na miti yenu yote, kwa maana Mwenyezi Mungu amemkomboa Yakobo, ameuonesha utukufu wake katika Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, kwa maana bwana amefanya jambo hili. Ee vilindi vya dunia, piga kelele. Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, enyi misitu na miti yenu yote, kwa maana bwana amemkomboa Yakobo, ameuonyesha utukufu wake katika Israeli. BIBLIA KISWAHILI Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli. |
Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha, Mbele za BWANA, Kwa maana anakuja kuihukumu nchi.
Na malisho yamejawa na kondoo, Na mabonde yamepambwa nafaka, Yanashangilia, na kuimba pamoja kwa shangwe.
Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
Yethro alifurahi kwa ajili ya wema wote BWANA aliowatendea Israeli, kwa alivyowaokoa mikononi mwa Wamisri.
Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.
Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.
Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.
Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.
Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu.
Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Wao ni chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, Kazi ya mikono yangu mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe.
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Kwa maana BWANA amemweka huru Yakobo, amemkomboa mkononi mwake aliyekuwa hodari kuliko yeye.
Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA.
Na wewe, mwanadamu, itabirie milima ya Israeli, useme, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la BWANA.
Lakini ninyi, enyi milima ya Israeli, mtachipuza matawi yenu na kuwapa watu wangu Israeli matunda yenu; maana wako karibu kuja.
Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU.
naam, atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.
Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?
Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.