Isaya 42:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu; utukufu wangu sitampa mwingine, wala sifa zangu sanamu za miungu. Biblia Habari Njema - BHND Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu; utukufu wangu sitampa mwingine, wala sifa zangu sanamu za miungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu; utukufu wangu sitampa mwingine, wala sifa zangu sanamu za miungu. Neno: Bibilia Takatifu “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu; hilo ndilo Jina langu! Sitampa mwingine utukufu wangu wala sanamu sifa zangu. Neno: Maandiko Matakatifu “Mimi ndimi bwana; hilo ndilo Jina langu! Sitampa mwingine utukufu wangu wala sanamu sifa zangu. BIBLIA KISWAHILI Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. |
Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.
Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.
ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.
Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.
Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.
basi nimekuonesha tangu zamani; kabla hayajatukia nilikuonesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru.
Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua.
BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi,
Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.
ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyemtuma.
Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;