Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
Isaya 42:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utayafumbua macho ya vipofu, utawatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru. Biblia Habari Njema - BHND Utayafumbua macho ya vipofu, utawatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utayafumbua macho ya vipofu, utawatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru. Neno: Bibilia Takatifu kuwafungua macho wale wasioona, kuwaacha huru kutoka kifungoni wale waliofungwa, na kuwafungua kutoka gerezani wale wanaokaa gizani. Neno: Maandiko Matakatifu kuwafungua macho wale wasioona, kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela, na kuwafungua kutoka gerezani wale wanaokaa gizani. BIBLIA KISWAHILI kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. |
Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.
Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.
kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza, Jionesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho.
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza.
Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea shutuma yangu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.
vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.
akamwambia, Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi akiwa anaona.
uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambaye amewanasa, hata wakayafanya mapenzi yake.
Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.