Isaya 42:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake yako wazi, lakini hasikii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyinyi mmeona mambo mengi, lakini hamwelewi kitu. Masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii kitu!” Biblia Habari Njema - BHND Nyinyi mmeona mambo mengi, lakini hamwelewi kitu. Masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii kitu!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyinyi mmeona mambo mengi, lakini hamwelewi kitu. Masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii kitu!” Neno: Bibilia Takatifu Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia; masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii chochote.” Neno: Maandiko Matakatifu Mmeona vitu vingi, lakini hamkuzingatia; masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii chochote.” BIBLIA KISWAHILI Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake yako wazi, lakini hasikii. |
Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.
Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu.
Naye akaniambia, Nenda, ukawaambie watu hawa, Endeleeni kusikia, lakini msifahamu; endeleeni kutazama, lakini msione.
Niseme na nani na kushuhudia, wapate kusikia? Tazama, sikio lao halikutahiriwa, wala hawawezi kusikiliza; tazama, neno la BWANA limekuwa matukano kwao; hawalifurahii.
Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.
Na tazama, wewe umekuwa kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga kinanda vizuri; maana, wasikia maneno yako, lakini hawayatendi.
kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;
Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe?
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;