Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Isaya 42:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Biblia Habari Njema - BHND Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Neno: Bibilia Takatifu Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataipaza sauti yake barabarani. Neno: Maandiko Matakatifu Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataiinua sauti yake barabarani. BIBLIA KISWAHILI Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. |
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatoa hukumu kwa uaminifu.
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.