Isaya 41:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, hao wote ni ubatili; kazi zao si kitu; sanamu zao ni upepo mtupu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema La! Miungu hiyo yote ni udanganyifu, haiwezi kufanya chochote; sanamu zao za kusubu ni upuuzi. Biblia Habari Njema - BHND La! Miungu hiyo yote ni udanganyifu, haiwezi kufanya chochote; sanamu zao za kusubu ni upuuzi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza La! Miungu hiyo yote ni udanganyifu, haiwezi kufanya chochote; sanamu zao za kusubu ni upuuzi. Neno: Bibilia Takatifu Tazama, wote ni ubatili! Matendo yao ni bure; vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama, wote ni ubatili! Matendo yao ni bure; vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko. BIBLIA KISWAHILI Tazama, hao wote ni ubatili; kazi zao si kitu; sanamu zao ni upepo mtupu. |
Wala hataziangalia madhabahu, kazi ya mikono yake; wala hatavitazama vilivyofanyika kwa vidole vyake, maashera na sanamu za jua.
Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyotengenezwa kwa vidole vyao wenyewe.
na kuwatupa miungu yao motoni; kwa maana hao hawakuwa miungu, bali kazi ya mikono ya wanadamu; walikuwa miti na mawe, ndiyo sababu wakawaharibu.
Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa kutoka kwa taabu yake.
Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa.
Sanamu ya kuchonga yafaa nini, baada ya aliyeifanya ameichonga? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini, hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanya sanamu zisizoweza kusema?
Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo watu wanatangatanga kama kondoo, wanateseka kwa kukosa mchungaji.
Na hao watu watano waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi wakakwea juu, wakaingia ndani, na kuitwaa hiyo sanamu ya kuchonga, na hiyo naivera, na kile kinyago, na hiyo sanamu ya kusubu; na huyo kuhani akasimama penye maingilio ya lango pamoja na hao wanaume mia sita waliojihami.