Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa kutoka kwa taabu yake.
Isaya 41:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na nitazamapo, hapana mtu, hata katika watu hao hapana mshauri mmoja, ambaye, nikimwuliza, aweza kunijibu neno. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimeangalia kwa makini sana, lakini simwoni yeyote yule; hamna yeyote kati ya hao miungu awezaye kushauri; nikiuliza hakuna awezaye kunijibu. Biblia Habari Njema - BHND Nimeangalia kwa makini sana, lakini simwoni yeyote yule; hamna yeyote kati ya hao miungu awezaye kushauri; nikiuliza hakuna awezaye kunijibu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimeangalia kwa makini sana, lakini simwoni yeyote yule; hamna yeyote kati ya hao miungu awezaye kushauri; nikiuliza hakuna awezaye kunijibu. Neno: Bibilia Takatifu Ninatazama, lakini hakuna yeyote: hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri, hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza. Neno: Maandiko Matakatifu Ninatazama, lakini hakuna yeyote: hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri, hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza. BIBLIA KISWAHILI Na nitazamapo, hapana mtu, hata katika watu hao hapana mshauri mmoja, ambaye, nikimwuliza, aweza kunijibu neno. |
Humchukua begani, humchukua, wakamsimamisha mahali pake, akasimama; hataondoka katika mahali pake, naam, mmoja atamwita, lakini hawezi kujibu, wala kumwokoa kutoka kwa taabu yake.
Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.
Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.
Nikatazama, wala hapakuwa na wa kunisaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia.
Basi wakaingia wenye hekima wote wa mfalme; lakini hawakuweza kuyasoma yale maandiko, wala kumjulisha mfalme tafsiri yake.