Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuoneshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye.
Isaya 41:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja aliyetuonesha; naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nani aliyebashiri haya tangu mwanzo, hata sisi tupate kuyatambua? Nani aliyetangulia kuyatangaza, ili sasa tuseme, alisema ukweli? Hakuna hata mmoja wenu aliyeyataja, wala hakuna aliyesikia maneno yenu. Biblia Habari Njema - BHND Nani aliyebashiri haya tangu mwanzo, hata sisi tupate kuyatambua? Nani aliyetangulia kuyatangaza, ili sasa tuseme, alisema ukweli? Hakuna hata mmoja wenu aliyeyataja, wala hakuna aliyesikia maneno yenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nani aliyebashiri haya tangu mwanzo, hata sisi tupate kuyatambua? Nani aliyetangulia kuyatangaza, ili sasa tuseme, alisema ukweli? Hakuna hata mmoja wenu aliyeyataja, wala hakuna aliyesikia maneno yenu. Neno: Bibilia Takatifu Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua, au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa mwenye haki’? Hakuna aliyenena hili, hakuna aliyetangulia kusema hili, hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu. Neno: Maandiko Matakatifu Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua, au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’? Hakuna aliyenena hili, hakuna aliyetangulia kusema hili, hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu. BIBLIA KISWAHILI Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja aliyetuonesha; naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu. |
Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuoneshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye.
Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.
Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.
Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze.
Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.
kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;