Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi, Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.
Isaya 41:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja; toka maawio ya jua amekuja anitajaye jina langu; naye atawakanyaga watawala kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi apondaye udongo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nimechochea mtu toka kaskazini, naye amekuja; naam, nimemchagua mtu toka mashariki, naye atalitamka jina langu. Yeye atawakanyaga wafalme kama tope, kama vile mfinyanzi apondavyo udongo wake. Biblia Habari Njema - BHND “Nimechochea mtu toka kaskazini, naye amekuja; naam, nimemchagua mtu toka mashariki, naye atalitamka jina langu. Yeye atawakanyaga wafalme kama tope, kama vile mfinyanzi apondavyo udongo wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nimechochea mtu toka kaskazini, naye amekuja; naam, nimemchagua mtu toka mashariki, naye atalitamka jina langu. Yeye atawakanyaga wafalme kama tope, kama vile mfinyanzi apondavyo udongo wake. Neno: Bibilia Takatifu “Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini, naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu. Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia. Neno: Maandiko Matakatifu “Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini, naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu. Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia. BIBLIA KISWAHILI Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja; toka mawio ya jua amekuja anitajaye jina langu; naye atawakanyaga watawala kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi apondaye udongo. |
Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi, Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.
Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.
Nimeoneshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote.
Ni nani aliyemwinua mmoja atokaye mashariki, ambaye katika haki amemwita mguuni pake? Ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme; awatoa wawe kama mavumbi kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake.
nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.
Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA wa majeshi.
Ndipo BWANA akaniambia, Toka kaskazini mabaya yatatokea, na kuwapata watu wote wakaao katika nchi hii.
Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.
Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi BWANA, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu.
Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu BWANA yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.
Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.