Isaya 41:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazameni, ninyi si kitu, tena kazi yenu si kitu; awachaguaye ninyi ni chukizo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakika, nyinyi si kitu kabisa. hamwezi kufanya chochote kile. Anayechagua kuwaabudu nyinyi ni chukizo. Biblia Habari Njema - BHND Hakika, nyinyi si kitu kabisa. hamwezi kufanya chochote kile. Anayechagua kuwaabudu nyinyi ni chukizo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakika, nyinyi si kitu kabisa. hamwezi kufanya chochote kile. Anayechagua kuwaabudu nyinyi ni chukizo. Neno: Bibilia Takatifu Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa, na kazi zenu hazifai kitu kabisa; yeye awachaguaye ni chukizo sana. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa, na kazi zenu hazifai kitu kabisa; yeye awachaguaye ni chukizo sana. BIBLIA KISWAHILI Tazameni, ninyi si kitu, tena kazi yenu si kitu; awachaguaye ninyi ni chukizo. |
na kuwatupa miungu yao motoni; kwa maana hao hawakuwa miungu, bali kazi ya mikono ya wanadamu; walikuwa miti na mawe, ndiyo sababu wakawaharibu.
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.
Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.
Lakini wote pia huwa kama wanyama, ni wapumbavu. Haya ni maelezo ya sanamu, ni shina la mti tu.
Basi kuhusu kuvila vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.
Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.
Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako;
na usitie kitu kilicho haramu ndani ya nyumba yako, usije ukalaaniwa kama haramu hiyo; ukichukie kabisa na kukikataa kabisa, kwa kuwa ni kitu kilicholaaniwa.
Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, Babeli MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.