Isaya 40:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Biblia Habari Njema - BHND Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Neno: Bibilia Takatifu Hata vijana huchoka na kulegea, nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka, Neno: Maandiko Matakatifu Hata vijana huchoka na kulegea, nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka, BIBLIA KISWAHILI Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka; |
Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Na nyuta zao zitawaangusha vijana; wala hawatahurumia mazao ya tumbo; jicho lao halitawahurumia watoto.
Kwa sababu hiyo Bwana hatawafurahia vijana wao, wala hatawahurumia yatima zao wala wajane wao; maana kila mtu ni mnajisi, dhalimu, na kila ulimi hunena upumbavu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wameteremka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.
Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.
Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu.
Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;
Lakini Daudi akaendelea kuwafuatilia, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori.