Isaya 40:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo, kwa nini mnalalamika na kusema: “Mwenyezi-Mungu hatujali sisi! Mungu wetu hajali haki yetu!” Biblia Habari Njema - BHND Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo, kwa nini mnalalamika na kusema: “Mwenyezi-Mungu hatujali sisi! Mungu wetu hajali haki yetu!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo, kwa nini mnalalamika na kusema: “Mwenyezi-Mungu hatujali sisi! Mungu wetu hajali haki yetu!” Neno: Bibilia Takatifu Kwa nini unasema, ee Yakobo, nanyi ee Israeli, kulalamika, “Njia yangu imefichwa Mwenyezi Mungu asiione, Mungu wangu hajali shauri langu?” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nini unasema, ee Yakobo, nanyi ee Israeli, kulalamika, “Njia yangu imefichwa bwana asiione, Mungu wangu hajali shauri langu?” BIBLIA KISWAHILI Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, BWANA asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? |
Ee BWANA, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.
Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.
Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu.
Kwa ghadhabu ifurikayo nilikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako.
Ndipo Daudi aliposema moyoni mwake, Siku moja, basi, mimi nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jema zaidi kwangu kuliko kukimbia mpaka nchi ya Wafilisti; naye Sauli atakata tamaa kunihusu, asinitafute tena kote mipakani mwa Israeli; hivyo nitaokoka katika mikono yake.