Isaya 40:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu, watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu. Biblia Habari Njema - BHND Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu, watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu, watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu. Neno: Bibilia Takatifu Huwafanya wakuu kuwa si kitu, na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure. Neno: Maandiko Matakatifu Huwafanya wakuu kuwa si kitu, na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure. BIBLIA KISWAHILI ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia. |
Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.
Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!
nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA.