Isaya 40:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Dunia iliumbwa na huyo aketiye juu ya mbingu; kutoka huko wakazi wa dunia ni kama panzi! Yeye amezitandaza mbingu kama pazia, na kuzikunjua kama hema la kuishi. Biblia Habari Njema - BHND Dunia iliumbwa na huyo aketiye juu ya mbingu; kutoka huko wakazi wa dunia ni kama panzi! Yeye amezitandaza mbingu kama pazia, na kuzikunjua kama hema la kuishi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Dunia iliumbwa na huyo aketiye juu ya mbingu; kutoka huko wakazi wa dunia ni kama panzi! Yeye amezitandaza mbingu kama pazia, na kuzikunjua kama hema la kuishi. Neno: Bibilia Takatifu Anakaa kwenye kiti cha utawala juu ya duara ya dunia, nao watu wanaoishi humo ni kama panzi. Huzitandaza mbingu kama chandarua, na kuzitandaza kama hema la kuishi. Neno: Maandiko Matakatifu Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia, nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi. Huzitandaza mbingu kama chandarua, na kuzitandaza kama hema la kuishi. BIBLIA KISWAHILI Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; |
Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Akiwa katika giza la mawingu mazito yaliyojaa maji.
Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema,
Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.
Ee BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia. Wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.
Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.
Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.
BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?
Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?
Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.