Isaya 40:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sanamu! Fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, anafanana na kinyago? Hicho, fundi hukichonga, mfua dhahabu akakipaka dhahabu, na kukitengenezea minyororo ya fedha! Biblia Habari Njema - BHND Je, anafanana na kinyago? Hicho, fundi hukichonga, mfua dhahabu akakipaka dhahabu, na kukitengenezea minyororo ya fedha! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, anafanana na kinyago? Hicho, fundi hukichonga, mfua dhahabu akakipaka dhahabu, na kukitengenezea minyororo ya fedha! Neno: Bibilia Takatifu Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu, naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu na kuitengenezea mikufu ya fedha. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu, naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu na kuitengenezea mikufu ya fedha. BIBLIA KISWAHILI Sanamu! Fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha. |
Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojitengenezea ili kuziabudu, kwa fuko na popo;
Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyotengenezwa kwa vidole vyao wenyewe.
Nanyi mtakitia najisi kifuniko cha sanamu zenu za fedha zilizochongwa, na mabamba ya sanamu zenu za dhahabu zilizoyeyushwa; utazitupilia mbali kama kitu kilicho najisi; utasema, Haya, toka hapa.
Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi, kazi ya fundi stadi na ya mikono ya mfua dhahabu; mavazi yao ni rangi ya samawati na urujuani; hayo yote ni kazi ya mafundi wao.
Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.
Maana katika Israeli kimetokea hata na kitu hiki; fundi ndiye aliyekifanya, nacho si mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande.
Basi hapo alipomrudishia mama yake hizo fedha, mama yake akatwaa fedha mia mbili, akampa fundi mwenye kusubu fedha, naye akafanya sanamu ya kuchonga kwazo, na sanamu ya kusubu; ambazo zilikuwa ndani ya nyumba ya Mika.