Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Isaya 38:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuutumainia uaminifu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huko kuzimu mtu hawezi kukushukuru wewe; waliokufa hawawezi kukushukuru wewe. Wala washukao huko shimoni hawawezi tena kutumainia uaminifu wako. Biblia Habari Njema - BHND Huko kuzimu mtu hawezi kukushukuru wewe; waliokufa hawawezi kukushukuru wewe. Wala washukao huko shimoni hawawezi tena kutumainia uaminifu wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huko kuzimu mtu hawezi kukushukuru wewe; waliokufa hawawezi kukushukuru wewe. Wala washukao huko shimoni hawawezi tena kutumainia uaminifu wako. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana kaburi haliwezi kukusifu, mauti haiwezi kuimba sifa zako; wale wanaoshuka shimoni hawawezi kuutarajia uaminifu wako. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana kaburi haliwezi kukusifu, mauti haiwezi kuimba sifa zako; wale washukao chini shimoni hawawezi kuutarajia uaminifu wako. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuutumainia uaminifu wako. |
Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo Shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yatautangaza uaminifu wako?
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wakiwa hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.
Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.