Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole.
Isaya 38:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini niseme nini: Yeye mwenyewe aliniambia, naye mwenyewe ametenda hayo. Usingizi wangu wote umenitoroka kwa sababu ya uchungu moyoni mwangu. Biblia Habari Njema - BHND Lakini niseme nini: Yeye mwenyewe aliniambia, naye mwenyewe ametenda hayo. Usingizi wangu wote umenitoroka kwa sababu ya uchungu moyoni mwangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini niseme nini: yeye mwenyewe aliniambia, naye mwenyewe ametenda hayo. Usingizi wangu wote umenitoroka kwa sababu ya uchungu moyoni mwangu. Neno: Bibilia Takatifu Lakini niseme nini? Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili. Nitatembea kwa unyenyekevu katika miaka yangu yote kwa sababu ya haya maumivu makali ya nafsi yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini niseme nini? Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili. Nitatembea kwa unyenyekevu katika miaka yangu yote kwa sababu ya haya maumivu makali ya nafsi yangu. BIBLIA KISWAHILI Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu. |
Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole.
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Nayachukia maisha yangu; Nitayasema malalamiko yangu wazi; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.
Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.