Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe; Kuna nani atakayeniwekea dhamana?
Isaya 38:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Ninalia kama mbayuwayu, nasononeka kama njiwa. Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu. Ee Bwana, nateseka; uwe wewe usalama wangu! Biblia Habari Njema - BHND “Ninalia kama mbayuwayu, nasononeka kama njiwa. Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu. Ee Bwana, nateseka; uwe wewe usalama wangu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Ninalia kama mbayuwayu, nasononeka kama njiwa. Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu. Ee Bwana, nateseka; uwe wewe usalama wangu! Neno: Bibilia Takatifu Nililia kama mbayuwayu au korongo, niliomboleza kama hua aombolezaye. Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni. Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!” Neno: Maandiko Matakatifu Nililia kama mbayuwayu au korongo, niliomboleza kama hua aombolezaye. Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni. Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!” BIBLIA KISWAHILI Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu. |
Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe; Kuna nani atakayeniwekea dhamana?
Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu.
Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi.
Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa.
Lakini watakaokimbia watakimbia, nao watakuwa juu ya milima kama hua wa bondeni, wote wakilia, kila mmoja katika uovu wake.
Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipigapiga vifua vyao.
Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma.