Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.
Isaya 37:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimechimba na kunywa maji, na kwa nyayo za miguu yangu nitaikausha mito yote ya Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimechimba visima na kunywa maji yake, na nilikausha vijito vya Misri kwa nyayo za miguu yangu.’ Biblia Habari Njema - BHND Nimechimba visima na kunywa maji yake, na nilikausha vijito vya Misri kwa nyayo za miguu yangu.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimechimba visima na kunywa maji yake, na nilikausha vijito vya Misri kwa nyayo za miguu yangu.’ Neno: Bibilia Takatifu Nimechimba visima katika nchi za kigeni na kunywa maji yake. Kwa nyayo za miguu yangu nimekausha vijito vyote vya Misri.’ Neno: Maandiko Matakatifu Nimechimba visima katika nchi za kigeni na kunywa maji yake. Kwa nyayo za miguu yangu nimekausha vijito vyote vya Misri.’ BIBLIA KISWAHILI Nimechimba na kunywa maji, na kwa nyayo za miguu yangu nitaikausha mito yote ya Misri. |
Ndipo Ben-hadadi akatuma kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.
Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa.
Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kiota cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia.
Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka.
Lakini yule kamanda akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma niseme, maneno haya kwa bwana wako na kwako wewe? Hakunituma pia kwa watu hawa wanaokaa ukutani, wanaokabiliwa na tisho la kula mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?
Kwa kuwa nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinyunyizia maji kwa mguu wako, kama shamba la mboga;