Akawafukuza mataifa mbele yao, Akawapimia urithi kwa kamba, Na kuwakalisha makabila ya Israeli katika hema zao.
Isaya 34:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye amewapigia kura, na mkono wake umewagawanyia kwa kamba; wataimiliki hata milele, watakaa ndani yake kizazi hata kizazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu amepanga sehemu ya kila mmoja wao, ametumia kamba kuwapimia nchi hiyo; wataimiliki milele na milele, wataishi humo kizazi hata kizazi. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu amepanga sehemu ya kila mmoja wao, ametumia kamba kuwapimia nchi hiyo; wataimiliki milele na milele, wataishi humo kizazi hata kizazi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu amepanga sehemu ya kila mmoja wao, ametumia kamba kuwapimia nchi hiyo; wataimiliki milele na milele, wataishi humo kizazi hata kizazi. Neno: Bibilia Takatifu Huwagawia sehemu zao, mkono wake huwagawanyia kwa kipimo. Wataimiliki hata milele na kuishi humo kizazi hadi kizazi. Neno: Maandiko Matakatifu Huwagawia sehemu zao, mkono wake huwagawanyia kwa kipimo. Wataimiliki hata milele na kuishi humo kutoka kizazi hadi kizazi. BIBLIA KISWAHILI Naye amewapigia kura, na mkono wake umewagawanyia kwa kamba; wataimiliki hata milele, watakaa ndani yake kizazi hata kizazi. |
Akawafukuza mataifa mbele yao, Akawapimia urithi kwa kamba, Na kuwakalisha makabila ya Israeli katika hema zao.
Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.
Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang'anya mali zetu.
Haitazimwa mchana wala usiku, moshi wake utapaa milele; tangu kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa; hapana mtu atakayepita kati yake milele na milele.
Kozi na nungunungu wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timazi ya utupu.
Hiyo ndiyo kura yako, fungu lako ulilopimiwa na mimi, asema BWANA; kwa kuwa umenisahau, na kuutumainia uongo.
Na alipokwisha kuwaangamiza mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini;
Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
Basi watu hao wakainuka wakaenda; Yoshua aliwaagiza wale waliokwenda kuichunguza nchi, akawaambia, Nendeni, mkapite katikati ya nchi, na kuandika habari zake, kisha mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za BWANA huko Shilo.