Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Isaya 3:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na pete za masikio, na vikuku, na mataji yao; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema vipuli, vikuku, shungi, Biblia Habari Njema - BHND vipuli, vikuku, shungi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza vipuli, vikuku, shungi, Neno: Bibilia Takatifu vipuli, vikuku, shela, Neno: Maandiko Matakatifu vipuli, vikuku, shela, BIBLIA KISWAHILI na pete za masikio, na vikuku, na mataji yao; |
Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Ikawa, alipoiona ile pete, na vikuku mikononi mwa dada yake, akasikia maneno ya Rebeka dada yake, akisema, Hivyo ndivyo alivyoniambia mtu huyo, basi akamjia mtu yule, na tazama, amesimama karibu na ngamia kisimani.
Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia.
Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na vipuli vilivyokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.
Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya mhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba.
Alipotolewa, alituma watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii.
Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mniletee.
Nao wakaja, wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, hazama, pete za mhuri, vikuku na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA.
Nikatia kishaufu puani mwako, na herini masikioni mwako, na taji zuri juu ya kichwa chako.
Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za mhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya BWANA.