Isaya 29:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, na wanaomwudhi, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalemu, wote wanaoshambulia ngome yake na kuutia wasiwasi, watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku. Biblia Habari Njema - BHND Hapo, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalemu, wote wanaoshambulia ngome yake na kuutia wasiwasi, watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalemu, wote wanaoshambulia ngome yake na kuutia wasiwasi, watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku. Neno: Bibilia Takatifu Kisha makundi ya mataifa yote yanayopigana dhidi ya Arieli, yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzingira kwa jeshi, watakuwa kama ilivyo ndoto, kama maono wakati wa usiku: Neno: Maandiko Matakatifu Kisha makundi ya mataifa yote yale yapiganayo dhidi ya Arieli, yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzunguka kwa jeshi, watakuwa kama ilivyo ndoto, kama maono wakati wa usiku: BIBLIA KISWAHILI Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, na wanaomwudhi, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku. |
Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang'anya mali zetu.
Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.
Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.
Yeye apondaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.
Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitayaangamiza mataifa yote yatakayokuja kupigana na Yerusalemu.