Isaya 29:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong'ona toka mavumbini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utaangushwa mbali sana ndani ya ardhi; kutoka huko mbali utatoa sauti; maneno yako yatatoka huko chini mavumbini; sauti yako itatoka ardhini kama ya mzimu. Biblia Habari Njema - BHND Utaangushwa mbali sana ndani ya ardhi; kutoka huko mbali utatoa sauti; maneno yako yatatoka huko chini mavumbini; sauti yako itatoka ardhini kama ya mzimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utaangushwa mbali sana ndani ya ardhi; kutoka huko mbali utatoa sauti; maneno yako yatatoka huko chini mavumbini; sauti yako itatoka ardhini kama ya mzimu. Neno: Bibilia Takatifu Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini, utamumunya maneno yako kutoka mavumbini. Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu, utanong’ona maneno yako toka mavumbini. Neno: Maandiko Matakatifu Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini, utamumunya maneno yako kutoka mavumbini. Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu, utanong’ona maneno yako toka mavumbini. BIBLIA KISWAHILI Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong'ona toka mavumbini. |
Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wakayachukiza macho ya utukufu wake.
Lakini mvua ya mawe itanyesha, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika.
nami nitalitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.
Jikung'ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungue vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa.
Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.