Isaya 29:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana mwenye kutisha ameangamizwa, naye mwenye dharau amekoma, nao wote watazamiao uovu wamekatiliwa mbali; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Majitu makatili yataangamizwa, wenye kumdhihaki Mungu watakwisha, wote wanaootea kutenda maovu watatokomezwa. Biblia Habari Njema - BHND Majitu makatili yataangamizwa, wenye kumdhihaki Mungu watakwisha, wote wanaootea kutenda maovu watatokomezwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Majitu makatili yataangamizwa, wenye kumdhihaki Mungu watakwisha, wote wanaootea kutenda maovu watatokomezwa. Neno: Bibilia Takatifu Wakatili watatoweka na wenye kudhihaki watatokomea, nao wote wenye jicho la uovu watakatiliwa mbali, Neno: Maandiko Matakatifu Wakatili watatoweka na wenye kudhihaki watatokomea, nao wote wenye jicho la uovu watakatiliwa mbali, BIBLIA KISWAHILI Kwa maana mwenye kutisha ameangamizwa, naye mwenye dharau amekoma, nao wote watazamiao uovu wamekatiliwa mbali; |
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;
Mimi mwenyewe nimewaamuru watu wangu waliowekwa wakfu kwangu, naam, nimewaita watu wangu walio hodari kwa ajili ya hasira yangu, watu wangu wenye kiburi.
Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi laini, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafla.
Naam, BWANA asema hivi, Hata mateka wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka wake aliye katili wataokoka; kwa maana nitapambana na yeye abishanaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.
Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?
Hakuna anayeshitaki kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.
Basi BWANA asema hivi, Angalia, nakusudia jambo baya juu ya jamaa hii, ambalo hamtazitoa shingo zenu, wala hamtakwenda kwa kiburi; kwa maana ni wakati mbaya.
Basi Herode akamdhalilisha, pamoja na askari wake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake.
Na Waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kama ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia.
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.